IQNA

Uislamu, dini rasmi Bangladesh

13:55 - June 23, 2011
Habari ID: 2143131
Uislamu utaendelea kuwa dini rasmi ya Bangladesh licha ya njama kubwa zilizofanywa na makundi mbalimbali za kuifanya nchi hiyo kuwa ya kisekulari.
Serikali ya Bangladesh imetangaza baada ya kuchunguza mapendekezo ya marekebisho ya katiba ya nchi hiyo kwamba nafasi ya Uislamu kama dini rasmi ya Bangladesh haitabadilika katika katiba mpya.
Mwaka 1972 ilitangazwa katika rasimu ya katiba kwamba Bangladesh ni nchi ya kisekulari lakini suala hilo lilibadilishwa katika mwaka 1988 na Uislamu ukatangazwa kuwa ndiyo dini rasmi ya nchi hiyo.
Wakati wa udhibiti wa Uingereza katika bara Hindi, Bangladesh ilijulikana kama Pakistan ya Kati na mwaka 1971 nchi hiyo ilitangaza uhuru na kujitenga na Pakistan baada ya miaka mingi ya vita vya ndani. 813277
captcha