Shirika la habari la Imarati WAM limeripoti kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Waqfu na Masuala ya Kheri ya nchi hiyo Muhammad Abid al Mazrui amesema misikiti hiyo mipya itajengwa kwa lengo ya kuboresha hali ya watu wanaokwenda kutekeleza ibada ya swala.
Amesema misikiti 8 itajengwa katika eneo la Bani Yas, 16 katika eneo la Magharibi, 8 huko al Ain, 20 Sharja, 18 Ajman, 12 Fujaira, 9 katika eneo la Umm al Qaiwin, 27 Raasul Khaima, na 8 katika eneo la Khur Fakan.
Ameongeza kuwa msikiti mmoja wa Fujaira na mingine 9 ya Raasul Khaima itakarabatiwa. 816686