IQNA

Wapinzani wa Uislamu wafeli tena Ufaransa

18:42 - July 03, 2011
Habari ID: 2148287
Maandamano ya makundi ya wabaguzi na wapinzani dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa yalifutwa jana kabla ya kufanyika.
Kituo cha habari cha Saphirnews kimeripoti kuwa maandamano ya kwanza ya makundi ya kibaguzi ya Ulaya na Marekani yalifutwa jana na vyombo vya sheria nchini Ufaransa.
Vilevile mkuu wa shule ya Kikatoliki ya Ufaransa amezuia mkutano wa makundi yanayohujumu Uislamu kwa hoja kwamba maudhui ya mkutano huo inakinzana na misingi ya Kikristo.
Makundi hayo sasa yanapanga kuitisha maandamano kama hayo wakati mwingine.
Makundi yanayoendesha hujuma dhidi ya Uislamu barani Ulaya na Marekani yalipanga kufanya maandamano jana mjini Strasbourg Ufaransa baada ya mkutano wa kujadili njia za kukabiliana na kasi ya kueneza dini ya Kiislamu kote duniani. 818905
captcha