Kituo cha habari cha Mondial-infos kimeripoti kuwa raia Waislamu na Wasiokuwa Waislamu wa Ubelgiji walifanya maandamano jana mjini Brussels na kutoa wito wa kuvunjwa mzingiro wa Gaza. Maandamano hayo yametayarishwa ya Jumuiya ya Ubelgiji kwa Ajili ya Gaza.
Wanachama wa jumuiya hiyo wamesema serikali ya Ugiriki imezuia msafara huo kuelekea Gaza kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya na kutokana na mashinikizo ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Ikumbukwe kuwa msafara wa Uhuru -2 unaobeba misaada ya kibinadamu kwa ajili ya raia wa Ukanda wa Gaza huko Palestina ambao unajumuisha meli 10 ulipaswa kuondoka bandari ya Ugiriki siku kadhaa zilizopita lakini safari hilo imekwamishwa na serikali ya Athens.
820232