Sheikh Salah ataachiwa huru Jumatatu ya wiki hii kutoka jela ya London. Jaji wa Mahakama ya London alisema jana baada ya kusikiliza ushahidi wa pande mbalimbali kwamba hakuna sababu yote inayothibitisha kwamba kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina ni tishio kwa usalama wa Uingereza.
Sheikh Raid Salah alikamatwa na vyombo vya usalama vya Uingereza wiki mbili zilizopita kwa tuhuma kwamba ni tishio kwa usalama wa nchi hiyo.
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina yuko nchi Uingereza kwa lengo la kushiriki kwenye kongamano la Siku ya Palestina. 826601