IQNA

Kanali ya Redio ya Haram ya Imam Ali (as) yafunguliwa Najaf

18:01 - July 18, 2011
Habari ID: 2155983
Matangazo ya majaribio ya Kanali ya Redio ya Haram ya Imam Ali bin Abi Twalib (as) ilifunguliwa jana kwa kipindi cha majaribio katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq.
Kanali hiyo ya redio ilifunguliwa jana sambamba na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Imam wa Zama Mahdi (as) na kipindi chake cha kwanza kilirushwa hewani kutoka ndani ya Haram Tukufu ya Imam Ali bin Abi Twalib (as).
Afisa anayeshughulikia masuala ya kifikra na kiutamaduni wa Haram ya Imam Ali (as) Hashim al Bachachi amesema kuwa Kanali ya Redio ya Haram ya Imam (as) imeanza kurusha matangazo ya majaribio ya masaa manne kwa siku.
Amesema matangazo hayo ya majaribio yataendelewa kwa kipindi cha wiki mbili na matangazo ya masaa 12 ya kanali hiyo yataanza mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Amesema vipindi vya redio hiyo vitahusu dini, utamaduni, fikra za Ahlul Bait (as), tafsiri ya Qur'ani, Hadithi na masuala ya kiitikadi.
Vilevile itarusha hewani vipindi vya masuala ya kijamii. Ameongeza kuwa televisheni ya mji mtakatifu wa Najaf pia itafunguliwa katika mwezi ujao wa Ramadhani.
827488
captcha