Masomo hayo yatawashirikisha walimu wa lugha za Kiarabu na Kifaransa wa mji wa Sikaso na yataendelea kwa kipindi cha siku tatu.
Hujjatul Islam Walmuslimin Ibrahim Samaki mwakilishi wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo la Sikaso nchini Mali amesema masomo mengine kama hayo yatatolewa nchini kote Mali kabla kidogo ya kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Walimu 40 wa lugha za Kiarabu na Kifaransa wa eneo la Sikaso watashiriki katika mafunzo elimu na maarifa ya Ahlul Bait (as). Duru ya kwanza ya mafunzo hayo ilifanyika mwaka jana chini ya usimamizi wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mali. 827668