Ayatullah Najafi alitoa matamshi hayo jana mjini Najaf katika mazungumzo yake na balozi wa Ufaransa nchini Iraq Bwana Denis Gauer. Ameitaka Ufaransa kutazama upya sheria hiyo inayowazuia wanawake wa Kiislamu kuingia mashuleni au katika ofisi za serikali ya nchi hiyo wakiwa na vazi la hijabu.
Sheikh Ali Najafi msemaji wa Ayatullahil Udhma Bashir Najafi amesema kuwa mazungumzo kati ya mwanazuoni huyo mkubwa na balozi wa Ufaransa nchini Iraq yaliendelea kwa kipindi cha saa nzima na kwamba pande hizo mbili zimejadili masuala yanayohusiana na Iraq, biashara na uchumi wa nchi hizo mbili. Amesema pande hizo pia zilijadili marufuku ya hijabu ya Kiislamu nchini Ufaransa na udharura wa kufutwa marufuku hiyo ambayo ni kinyume na demokrasia ya nchi za Magharibi inayoruhusu uhuru wa mtu binafsi. 827977