CAIR imesema kuwa mazungumzo kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu ndiyo njia bora zaidi ya kukabiliana na ongezeko la hujuma ya propaganda chafu dhidi ya Uislamu na Waislamu duniani na limewataka wasimamizi wa misikiti wafungue wazi milango ya vituo vya ibada kwa ajili ya wasiokuwa Wislamu katika mwezi ujao wa Ramadhani.
Sehemu moja ya taarifa ya CAIR imesema watu wasiokuwa Waislamu ambao wanasuhubiana na Waislamu wana mitazamo ya wastani kuhusu dini ya Kiislamu na kwa kawaida huwa hawatoi maoni yasiyokuwa na maana kuhusu dini hiyo.
Taarifa hiyo imesema kuwepo Wasiokuwa Waislamu katika chakula cha futari ya mwezi mtukufu wa Ramadhani misikitini ndiyo njia bora zaidi ya mazungumzo kati ya watu hao na Waislamu na njia muafaka ya kukabiliana na propaganda za kuwatisha watu kuhusu dini ya Kiislamu. 828604