Ukurasa wa mtandao wa intaneti wa Islam Today umeripoti kuwa kitabu hicho kilichopewa jina la Uhakika Kuhusu Funga ya Mwezi wa Ramadhani' kimechapishwa na British Health Foundation na kinapatikana pia katika mtandao wa intaneti wa jumuiya hiyo.
Daktari Winod Patel wa hospitali ya George Eliot katika mji wa Nuneaton amesema mwaka huu funga ya siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani mjini London itaanza saa 3:53 alfajiri na kumalizika saa 2:49 usiku. Anasema muda wa funga utakuwa karibu masaa 17 ambayo ni tatizo kwa watu wenye maradhi ya kisukari.
Daktari huyo anasema watu wenye maradhi ya kisukari wanapaswa kubadilisha wakati wa kutumia dawa zao katika mwezi wa Ramadhani iwapo watataka kufunga saumu ili wasikabiliwe na matatizo makubwa kama shinikizo la damu na kupoteza fahamu.
Amesema kuwa kitabu hicho kinatoa mafunzo na muongozo kwa wagonjwa wa kisukari juu ya namna ya kulinda afya zao wakati wanapokuwa katika saumu. 828816