IQNA

Mpango wa "Ramadhani 2011" kutekelezwa Senegal

18:51 - July 27, 2011
Habari ID: 2161122
Jumuiya ya Misaada ya Kiislamu ya Ufaransa (Secours Islamique France) imeazimia kutekeleza mpango wa 'Ramadhani 2011' katika siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Senegal.
Jumuiya hiyo imetangaza kuwa itagawa chakula kwa familia za Waislamu katika miji ya Dakar, Tambacounda na Kaolack katika mwezi wa Ramadhani.
Misaada hiyo itatolewa katika utekelezaji wa mpangp wa "Ramadhani 2011" na itahusu familia zaidi ya 1500 zisizojiweza na zisizokuwa na wasimamizi.
Wizara ya Masuala ya Kijamii ya Senegal, Jumuiya ya Umoja wa Kitaifa, viongozi wa serikali ya Dakar, maimamu wa swala za jamaa na wanachama wa jumuiya za misaada za Kiislamu za Ufaransa wanashirikiana katika kutekeleza mpango huo. 832389
captcha