Chama cha Umma ambacho ni miongoni mwa vyama vinavyoipinga serikali ya kifalme ya Saudi Arabia kimewataka maulamaa wa Kiislamu kulalamikia sheria hiyo.
Serikali ya Saudia inapiga marufuku kuasisi chama cha kisiasa au upinzani wowote wa kisiasa dhidi ya serikali.
Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limechapisha nakala ya sheria ya kupambana na ugaidi iliyopasishwa na seriikali ya Saudi Arabia na kuandika kuwa sheria hiyo inaipa serikali ruhusa ya kuwatia nguvuni na kuwahukumu watu bila ya tuhuma yoyote na kuzuia maandamano ya amani.
Kwa mujibu wa sheria hiyo mpya, raia yeyote anayemkosoa mfalme wa Saudi Arabia atakabiliwa na tuhuma za kuvuruga umoja wa kitaifa, kuvunjia heshima serikali na kufanya jinai ya ugaidi. Adhabu ya chini kabisa ya tuhuma kama hizo ni kifungo cha miaka 10 jela. 833423