IQNA

Kuhani amuombea msamaha Mubarak

15:10 - August 09, 2011
Habari ID: 2167936
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Taurati katika utawala ghasibu wa Israel amemtaka Sheikh wa al Azhar nchini Misri kutoa fatuwa ya kidini ya kumsamehe dikteta wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak.
Katika hatua ya aina yake kuhani Ofadia Joseph amemtaka Sheikh Ahmad al Tayyeb, mkuu wa al Azhar nchini Misri kutoa fatuwa ya kumsamehe rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak anayekabiliwa na mashtaka ya kuua na kutumia vibara madaraka.
Kuhani hiyo amesema katika hotuba rasmi kwamba viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanapasa kuishinikiza serikali ya Marekani ili iingilie kadhia ya kesi ya Hosni Mubarak na kuzuia kunyongwa dikteta huyo.
Kuhani huyo pia amemtaka Rais wa Israel Shimon Perez kuushawishi Umoja wa Ulaya ili uingilie kati na kumnusuru Hosni Mubarak.
Hatua hiyo ya kuhani wa Kiyahudi ni ya aina yake. Kuhani Ofadia Joseph ni miongoni mwa marafiki wakubwa wa dikteta aliyeng’olewa madarakani wa Misri Hosni Mubarak na amekuwa akimpongeza kila mwaka katika siku ya kuzaliwa kwake na kumtakia afya njema na mafanikio! 840238
captcha