IQNA

Thamani za Uislamu na Ukristo kuchunguzwa Misri

17:39 - August 16, 2011
Habari ID: 2172105
Kikao cha kuchunguza thamani za pamoja za Uislamu na Ukristo kitafanyika kesho katika Baitul Umma mjini Cairo, Misri.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utamaduni ya 'Sa'd Zaghlul', Tariq Maamun amesema kuwa kikao hicho kitafanyika kesho Jumatano kwa usimamizi wa taasisi hiyo na Kituo cha Mazungumzo cha Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al Azhar.
Amesema kikao hicho kitahutubiwa na wasomi, wanazuoni na wanafikra wa Kiislamu na Kikristo wa Misri.
Tariq Maamun ameongeza kuwa kandokando ya kikao hicho kutakuwepo maonyesho ya ada na Wamisri, sanaa za mikono, burudani za muziki na michezo ya kuigiza, usomaji wa tenzi za mashairi na ratiba nyingine kadhaa zitakazowashirikisha wasanii kutoka Sudan, Libya na Misri. 844552
captcha