IQNA

Semina ya ‘Nafasi ya Wanawake katika Uislamu’ yafanyika Senegal

11:59 - August 17, 2011
Habari ID: 2172237
Kikao kuhusu ‘Nafasi ya Wanawake katika Uislamu’ kimefanyika Agosti 16 katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.
Kikao hicho kimeandaliwa na Jumuiya ya Wanawake wa Morocco Waishio Senegal.
Kikao hicho kimefanyika baada ya futari katika Kituo cha Utamaduni cha Douta Seck mjini Dakar.
Maryam Drame mhadhiri wa Sayansi za Kiislamu amezungumza kuhusu nafasi ya wanawake katika jamii za Kiislamu. Ameashiria aya za Qur’ani na Hadithi za Mtume SAW kuhusu nafasi ya wanawake katika Uislamu. Aidha amezungumza kuhusu hali ya sasa ya wanawake katika umma wa Kiislamu.
Hafla hiyo imedhuhuriwa na takribani wanawake 300.
844238
captcha