Barza hilo litazijumuisha jumuiya, husseiniya na taasisi zote za Kiislamu zinazoendeshwa na Wairaqi. Akizungumzia suala hilo Wassam Said as-Saffar mkuu wa kitengo cha upashaji habari cha baraza hilo amesema kwamba wawakilishi wa mamarja' na wanazuoni mashuhuri wa Iraq akiwemo Ayatullah Sayyid Murtadha al- Kashmiri na Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Sistani wamezitembelea ofisi za baraza hilo huko Ujerumani. Wawakilishi hao wamejadiliana na kubadilishana mawazo na wakuu wa baraza hilo jinsi ya kuzihudumia kwa njia bora zaidi jumuiya za Kiislamu za Wairaki zinazopatikana katika miji tofauti ya Ujerumani.
As-Saffar amesema kuwa baraza hilo ni la pekee la aina yake katika nchi za Ulaya na kwamba lina mipango ya kuchapisha gazeti litakaloeneza mafundisho ya Ahlul Beit (as) nchini Ujerumani, ambalo litachapishwa kwa lugha mbili za Kiarabu na Kijerumani. 846091