IQNA

Mafunzo ya Qur'ani kufanyika Manchester

16:37 - November 28, 2011
Habari ID: 2230758
Vikao vya mafunzo ya kuzingatia Qur'ani Tukufu vitaanza kufanyika tarehe 2 Disemba katika mji wa Manchester kwa hima ya Jumuiya ya Kiislamu ya chuo kikuu cha mji huo.
Masomo ya kiraa sahihi ya Qur'ani Tukufu, mbinu za kuhifadhi Qur'ani, kuelewa maana na tafsiri ya Qur'ani Tukufu yatatolewa kwa washiriki katika masomo hayo.
Vikao hivyo vitakuwa vikifanyika katika siku za Jumatano na Alkhamisi ya kila wiki.
Jumuiya ya Kiislamu ya Manchester Jumamosi tarehe 26 Novemba pia ilikuwa na warsha iliyopewa jina la "Qur'ani: Ujumbe Usiokuwa na Zama Makhsusi", kwa shabaha ya kuchunguza ujumbe wa Mwenyezi Mungu Muumba. 906841
captcha