IQNA

Masomo ya muda ya tajwidi ya Qur'ani kwa ajili ya wanawake yaanza Palestina

17:00 - November 30, 2011
Habari ID: 2232261
Masomo ya muda ya sheria na kanuni za kiraa na tajwidi ya Qur'ani Tukufu yalianza jana Jumanne katika mji wa Nablos huko Palestina kwa hima ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya kidini.
Masomo hayo ambayo ni makhsusi kwa walimu wa malezi ya Kiislamu yataendelea kwa kipindi cha miezi saba.
Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Wanawake katika Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Palestina Maisara al Naubani amesema kuwa masomo hayo yanasimamiwa na wizara hiyo kwa lengo la kuboresha kiwango cha kiraa na tajwidi ya Qur'ani Tukufu katika jamii na kuimarisha uhusiano wa wanafunzi na kitabu cha Mwenyezi Mungu.
Amesema kuwa malengo mengine ya masomo hayo ni kufanya juhudi za kuwahamasisha wanafunzi kusoma na kuhifadhi Qur'ani, kuelewa maneno ya Mwenyezi Mungu na kufanyia kazi mafundisho yanayotoa uhai ya Qur'ani Tukufu. 908804

captcha