IQNA

Mafunzo ya Qur'ani kuchunguzwa Malaysia

16:37 - December 10, 2011
Habari ID: 2236118
Mafunzo ya Qur'ani na sayansi ya kitabu hicho yatachunguzwa katika warsha itakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu nchini Malaysia tarehe 12 na 13 Disemba.
Kituo cha habari cha Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu Malaysia (IIUM) kimeripoti kuwa warsha hiyo itafanyika kwa hima ya Jumuiya ya Kimataifa ya Umoja wa Waislamu.
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Kiislamu ISESCO na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhisha Qur'ani (HQMIO) zinashirikiana katika kusimamia warsha hiyo.
Warsha hiyo itachunguza njia za kustawisha mafunzo ya Qur'ani, kuzidisha nafasi ya teknolojia za kisasa kama intaneti na televisheni za satalaiti kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Qur'ani Tukufu, uchunguza wa kustawisha mbinu za kufunza Qur'ani na kadhalika. 912868

captcha