IQNA

Mafundisho ya Qur'ani kutolewa kwa Waislamu wapya Uingereza

16:47 - December 10, 2011
Habari ID: 2236123
Kituo cha Kiislamu cha Uingereza kimeanzisha masomo ya muda ya mafunzo ya Qur'ani na sheria za Kiislamu kwa Waislamu wapya mjini London.
Mafunzo ya lugha ya Kiarabu, sheria za fiqhi, maadili ya Kiislamu na kiraa ya Qur'ani Tukufu yanatolewa kwa wanawake na wanaume siku za Jumamosi katika masomo hayo ya muda.
Masomo ya kiraa ya Qur'ani Tukufu yatatolewa katika ngazi tatu za msingi, masomo ya kati na elimu ya juu.
Mafunzo hayo yanasimamiwa na kitengo cha lugha ya Kiingereza cha Kituo cha Kiislamu cha Uingereza kuanzia leo tarehe 10 Disemba na yataendelea hadi tarehe 26 Machi mwakani. 912804
captcha