IQNA

Kesi ya waliosambaza nakala zenye makosa ya chapa za Qur'ani yaahirishwa Misri

10:04 - December 11, 2011
Habari ID: 2236387
Mahakama ya Jinai ya Alexandria nchini Misri imeahirisha kikao cha kusikiliza kesi inayowakabili watu waliohusika na kusambaza nakala za Qur'ani Tukufu zenye makosa ya chapa hadi tarehe 28 Februari mwakani.
Gazeti la al Wafd limeripoti kuwa Mahakama ya Jinai ya Alexandria imeahirisha kesi ya wafanyabiashara wawili wa Kimisri wanaokabiliwa na tuhuma za kuuza na kusambaza nakala za Qur'ani zenye makosa ya uchapishaji.
Uamuzi wa kuahirishwa kesi hiyo uliuchukuliwa katika kikao cha mahakama kilichohudhuriwa na majaji Faruq Haridi na Mamduh Abdul Daim.
Awali kampuni moja ya kuzalisha rekodi za kidini ilikuwa imeituhumu Maktaba ya al Shahira kwamba imeuza nakala za Qur'ani zenye makosa ya kichapa na pia kuuza nakala 500 za kitabu hicho bila ya idhini ya al Azhar. Imedai kuwa baadhi ya aya za nakala hizo za Qur'ani zimefutwa.
Baada ya mashtaka hayo maktaba hiyo ilifungwa na wamiliki wake Abdul Muizz Mahmoud Muhammad na Husam Jabir Muhammad wakatiwa nguvuni. 912921



captcha