Mkutano huo unahudhuriwa na wasomi na shakhsia 30 kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Sayansi za Kiislamu cha Jordan Abdul Naseer Abul Fadhl amesema katika ufunguzi wa mkutano huo kwamba hii ni mara ya kwanza kwa mkutano wa Qur'ani Tukufu na Nafasi Yake katika Ustaarabu wa Kiislamu kufanyika Jordan na kuongeza kuwa lengo lake ni kufafanua na kubainisha juhudi zilizofanyika kulinda kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu tangu kiteremshwe hadi hii leo. Amesisitiza kuwa lengo jingine ni kubainisha kiwango cha taathira ya Qur'ani katika fasihi za Waislamu.
Washiriki katika mkutano huo pia watabadilishana mawazo na uzoefu katika masuala ya kuchapisha na kusambaza Qur'ani Tukufu kwa kutumia teknolojia mpya. 914895