Mashindano hayo yatafunguliwa katika kituo cha Raudha bint Muhammad mjini Doha.
Mashindano hayo yanawashirkisha makarii na wasomaji Qur'ani wa vituo vya Qur'ani vilivyo chini ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar na leo wasomaji 105 wanatazamiwa kuchuana.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo Khalid bin Muhammad Aal Thani amesema watu wengi wamekuwa wakivutiwa mno na mashindano hayo ya kitaifa ya Qur'ani na kwamba wasomaji wa kike na kiume walionyesha uwezo na vipawa vyao katika awamu ya kwanza ya mashindano hayo yaliyopewa jina la 'Sheikh Ghanim bin Ali'.
Sherehe ya kuhitimisha mashindano hayo itafanyika tarehe 28 Disemba katika Hoteli ya Ramada katika mji mkuu wa Qatar. 915758