IQNA

Ensaiklopidia ya ‘Sayansi za Qur’ani’ katika maonyesho Qatar

16:09 - December 17, 2011
Habari ID: 2239515
Ensaiklopidia ya sayansi za Qur’ani yenye kalamu erevu inayozungumza na yenye qiraa ya maqari 20 mashuhuri inaonyeshwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu huko Doha mji mkuu wa Qatar.
Kwa mujibu wa gazeti la Ar Rayah, Mohammad Saadi Al Mukhalalati Mkurugenzi wa Shirika la Uchapishaji na Usambazaji la Dar Ar-Rashid la Syria amesema ensaiklopidia hiyo ni ubunifu wa Hassan Hamisi anayesimamia taasisi hiyo.
Mvumbuzi wa kalamu hiyo erevu amesema kuwa inaweza kuboreshwa kupitia intaneti.
Ameongeza kuwa seti kamili ya ensaiklopidia hiyo inagharimu 350 Riyali za Qatari ikiwa ni pamoja na kalamu erevu.
Maonyesho hayo yalifunguliwa Disemba 12 katika sherehe zilizohudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran Dr. Sayyid Mohammad Husseini.
Mashirika na taasisi kadhaa za Iran zinashiriki katika maonyesho hayo ambayo yatadumu siku 10.
915630
captcha