IQNA

Mashindano ya 28 ya Qur'ani kufanyika Pakistan

18:56 - December 17, 2011
Habari ID: 2240209
Mashindano ya 28 ya Qur'ani Tukufu yatafanyika Jumatatu ijayo katika Msikiti wa Faisal Abad katika mkoa wa Punjab nchini Pakistan.
Mashindano hayo yanasimamiwa na Jumuiya ya Wakfu ya Punjab na yatafanyika katika sehemu mbili za hifdhi na kiraa ya Qur'ani.
Washiriki katika kitengo cha hifdhi watachuana katika kuhifadhi juzuu 30, 20, 10 na 5 za Qur'ani Tukufu.
Kitengo cha kiraa ambacho kitawashirikisha wanawake na wanaume, kitakuwa na sehemu mbili za watu wenye umri wa juu ya miaka 16 na chini ya umri huo. 917132
captcha