Mashindano ya 33 ya kimataifa ta hifdhi, tajwidi na tafsiri ya Qur'ani yamenza leo nchini Saudi Arabia chini ya usimamizi wa Wizara ya Wakfu, Tablighi na Miongozo ya nchi hiyo. Mashindano hayo yanafanyika katika Masjidul Haram mjini Makka.
Makari na mahafidhi 161 kutoka nchi 53 wanachuana katika mashindano hayo kwa kipindi cha wiki moja.
Wizara ya Wakfu ya Saudia imetangaza majina ya makari wanaoshiriki katika mashindano hayo ya kimataifa kwa niaba ya sekretarieti ya mashindano hayo.
Majaji 6 kutoka nchi za Misri, Jordan, Mauritania, Malaysia, Pakistan na Nigeria wanashirikiana na wenzao wanne wa Saudia kusimamia mashindano hayo ya kimataifa.
Washindi wa kwanza katika kila kitengo cha mashindano hayo watapewa tuzo ya kati ya riale laki moja na elfu 60.
Katibu Mkuu wa Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Saudi Arabia Mansour bin Muhammad amesema kuwa lengo lake ni kushajiisha vijana kusoma, kuhifadhi na kutadabari aya za kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu na kuimarisha moyo wa ushindani kati ya mahafidhi na makarii wa Qur'ani Tukufu.
Kandokando ya mashindano hayo kutakuwepo duru ya kimataifa ya masomo ya majaji wa Qur'ani tukufu. 917601