IQNA

Maonyesho ya Qur'ani yafanyika Australia

16:20 - December 20, 2011
Habari ID: 2241969
Maonyesho ya Qur'ani Tukufu kuhusu sanaa yamefanyika katika mji wa Cranbourne katika jimbo la Victoria nchini Australia.
Kwa mujibu wa tovuti ya Berwickleader.com, sanaa za Qur'ani, tarjumi za Qur'ani kwa lugha tofauti, johari na sanaa nyingine ambazo aya za Qur'ani zimeandikwa juu yake ni baadhi ya vitu vilivyoonyeshwa kwenye maonyesho hayo.
Nurein Chaudri mmoja wa waandaaji wa maonyesho hayo amesema kuwa wageni wengi wameyatembelea maonyesho hayo kuliko ilivyotazamiwa awali na kwamba mbali na mji wa Cranbourne, wageni wengi walitoka katika miji mingine ya mbali ikiwemo ya Sydney na Canberra. Amesema vikao viwili muhimu vilifanyika pambizoni mwa maonyesho hayo kuhusiana na Qur'ani Tukufu, sifa na historia yake.
Chaudri amesema kuwa lengo la kufanyika maonyesho hayo ni kunyanyua mwamko na ufahamu wa wafuasi wa dini tofauti za mbinguni kuhusu kitabu kitakatifu cha Waislamu yaani Qur'ani Tukufu, na wakati huohuo kuimarisha mazingira ya wafuasi wa dini hizo kuishi pamoja kwa amani.
Amesema waandaaji wa maonyesho hayo pia wanafanya juhudi za kuandaa maonyesho kama hayo katika miji mingine ya Australia. 919098
captcha