Mashindano hayo yatasimamiwa na Kituo cha Kiislamu cha Vermont kwa lengo la kuwahamasisha watoto kusoma Qur'ani na kutafakari aya za kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Mashindano hayo yatafanyika katika sehemu mbili za hifdhi ya sura za Nas hadi Kauthar, na hifdhi ya sura za Nas hadi Zilzal kwa watoto wenye chini ya umri wa miaka 8, na vitengo vitatu vya hifdhi ya nusu ya juzuu ya 30, juzuu nzima ya Amma, na hifdhi ya juzuu za 29 na 30 kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka 4 hadi 15.
Washiriki watachunguzwa kuhusu uwezo wao wa hifdhi na kutekeleza vyema kanuni za tajwidi na washindi wataenziwa kwa kutunukiwa zawadi. 919385