IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yamalizika Saudia

11:58 - December 25, 2011
Habari ID: 2244624
Sherehe za kuhitimisha duru ya tatu ya mashindano ya kimataifa ya hifdhi, tajwidi na tafsiri ya Qur'ani Tukufu zimepangwa kufanyika leo Jumapili katika Masjidul Haram nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa gazeti la Shams, sherehe hizo zitahudhuriwa na Khalid Faisal, Amir wa eneo la Makka, akimwakilisha mfalme wa Saudi Arabia, ambapo washindi wa mashindano hayo watatunukiwa zawadi.
Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Wizara ya Wakfu, Masuala ya Kiislamu, Uenezaji na Mwongozo ya Saudi Arabia yalianza tarehe 18 Disemba huko Masjidul Haram yakiwashirikisha washindani 161 kutoka nchi 53 za dunia.
Mashindano hayo yalifanyika katika makundi matano ya hifdhi ya Qur'ani nzima kwa kuzingatia sheria za tajwidi, tafsiri na maana ya aya, hifdhi ya Qur'ani nzima kwa kuzingatia tajwidi, hifdhi ya juzuu 20 mfululizo kwa kuzingatia sheria za tajwidi, hifdhi ya juzuu 10 mfululizo kwa kuzingatia sheria za tajwidi na hifdhi ya juzuu 5 mfululizo, maalumu kwa wasiokuwa Waislamu.
Washindi wa kwanza kutoka kila kundi wanatazamiwa kupewa zawadi ya riale za Saudia kati ya 60,000 hadi laki moja.
Wakati huohuo duru ya pili ya mafunzo ya kimataifa ya waamuzi wa mashindano ya Qur'ani ilifanyika pambizoni mwa mashindano hayo kwa lengo la kulea na kutayarisha waamuzi wanaofaa kwa ajili ya kusimamia na kutoa maamuzi katika mashindano mbalimbali ya Qur'ani Tukufu kitaifa na kimataifa. 921917
captcha