IQNA

Mashindano ya 12 ya Qur'ani Tukufu kufanyika Marekani

10:43 - December 26, 2011
Habari ID: 2245300
Mashindano ya 12 ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika mwezi Machi mwakani katika Kituo cha Kiislamu cha Masumeen kwenye eneo la New England huko Marekani.
Mashindano hayo ambayo yatasimamiwa na Kituo cha Kiislamu cha Masumeen na Jumuiya ya Kiislamu ya Waislamu wa New England yatafanyika kwa lengo la kutayarisha fursa ya kusoma, kuhifadhi na kujifunza maarifa ya Qur'ani Tukufu.
Mashindano hayo yatafanyika katika vitengo vitano vya hifdhi, kiraa, maarifa ya Qur'ani, kuhifadhi sura fupi na michoro inayohusiana na masuala ya Qur'ani.
Katika upande wa hifdhi, washindani watatakiwa kuhifadhi sura za Rahman, Saff na Infitar.
Washiriki katika kitengo cha kiraa, watachuana katika kusoma sura ya Aal Imran na kitengo cha michoro kiwashirikisha washindani wenye umri tofauti katika kuchora na kuandika masuala yanayohusiana na aya za Qur'ani Tukufu. 922353

captcha