IQNA

Kongamano la Vyombo vya Habari na Utamaduni wa Qur'ani kufanyika Iraq

22:22 - December 27, 2011
Habari ID: 2246599
Kongamano la Mchango wa Vyombo vya Habari katika Kueneza Utamaduni wa Qur'ani nchini Iraq utafanyika kesho katika mji wa Nasiriyya kwa ushirikiano wa Shirika la habari la IQNA.
Mkurugenzi wa Darul Qur'an al Karim katika mji wa Nasiriyya Raad Adnan amesema kuwa kongamano hilo litasimamiwa na Darul Qur'an al Karim ya mji huo ikishirikiana na shirika la habari la IQNA katika Chuo Kikuu ch Dhiqar.
Amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kueneza utamaduni wa Qur'ani katika jamii ya Iraq hususan katika kiwango cha vyuo vikuu. Amesema kongamano hilo litahudhuriwa na shakhsia na wasomi mashuhuri wa Iraq.
Amesema kuwa miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na uchunguzi kuhusu sababu muhimu zinazoathiri katika kueneza utamaduni wa Qur'ani katika jamii ya Iraq na njia za kuakisi maarifa na mafundisho ya Qur'ani kupitia vyombo vya habari. 923673
captcha