IQNA

Tafsiri ya Suratu Hud kuchunguzwa katika Chuo Kikuu cha London

15:39 - December 28, 2011
Habari ID: 2247091
Tafsiri ya sura tukufu ya Hud imepangwa kuchunguzwa hivi karibuni katika Chuo cha Queen Mary katika Chuo Kikuu cha London.
Kwa mujibu wa tovuti ya IIDR kikao cha kielimu cha kuchunguza tafsiri hiyo kimeandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Ustawi na Utafiti ya London. Kikao hicho kimepangwa kufanyika tarehe 14 Januari kwa lengo la kuchunguza maana na pande mbalimbali za sura hiyo ya 11 ya Qur'ani Tukufu.
Adam Jamal Mwislamu wa Marekani aliyesomea masuala ya sheria za Kiislamu ambaye pia ni mhadhiri wa masomo ya Kiislamu atazungumza na kutoa tafsiri ya sura hiyo.
Mapema mwezi huu, Taasisi ya Kiislamu ya Ustawi na Utafiti ya London iliandaa warsha ya masomo ya siku nne katika chuo hichohicho kwa madhumuni ya kuchunguza maisha na mafundisho ya Mtume Mtukufu (saw).
Taasisi hiyo huandaa kikao kimoja au viwili kila mwezi kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Qur'ani na masomo mbalimbali ya Kiislamu kwa wale wanaotaka kunufaika na masomo hayo. 924396
captcha