Kwa mujibu wa gazeti la Al Shoruq,tarjumi hiyo ilianza kuandikwa na Ahmed Hamed muasisi wa taaluma ya mikrobiolojia nchini Misri. Mwanaye, Mohammad Hamed alifanya hima na kukamilisha kazi hii yenye thawabu iliyokuwa imeanzishwa na baba yake.
Mohammad Hamed alizaliwa mwaka 1928 na baadaye akahitimui kuwa daktari mtaalamu wa watoto na kisha akawa mkuu wa Akademia ya Tiba ya Jeshi la Misri.
Katika kutarjumi ya Qur'ani, Mohammad Hamed ametegemea tafsiri za wanazuoni wa ngazi za juu.
Tarjumi hii mpya ya Qur'ani imechapishwa chini ya usimamizi wa Taasisi ya Utafiti, Uandishi na Tarjumi. Taasisi hii inafungamana na Chuo Kikuu cha Al Azhar.
925510