IQNA

Mashindano ya kitaifa ya kiraa ya Qur'ani yakamilika Uchina

14:44 - December 31, 2011
Habari ID: 2248252
Duru ya 9 ya mashindano ya kitaifa ya kiraa ya Qur'ani Tukufu ilikamilika siku ya Alkhamisi huko Peking mji mkuu wa China.
Kwa mujibu wa tovuti ya arabic1.peoplel.com, makari 60 kutoka mikoa 23 na maeneo ya utawala wa ndani walishiriki katika mashindano hayo ya kitaifa yaliyofanyika katika Kituo cha Utafiti wa Kiislamu cha China.
Washiriki wa mashindano hayo walitoka makabila, jamii na kaumu tofauti za China, ambapo mshindi wa kwanza wa Mashindano hayo alikuwa ni Wali Mahsuti kutoka katika mji wa Shengyan katika mkoa wa Henan.925497
captcha