Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Morocco imetangaza kuwa mashindano hayo ya Qur'ani yatafanyika sambamba na sherehe za maualidi ya kuzaliwa mtume Muhammad (saw)
Taarifa ya wizara hiyo imesema kuwa sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zitahudhuriwa na wawakilishi wa nchi mbalimbali katika Msikiti wa Hussan wa Pili mjini Casablanca.
Ni vyema kusema hapa kuwa vijana kutoka nchi 33 duniani walichuana katika mashindano ya kimataifa ya sita ya Qur'ani yaliyopewa jina la Tuzo ya Mfalme Muhammad wa Sita.
Majaji 6 wa Morocco na wengine kutoka nchi za Libya, Misri, Saudi Arabia na Jordan watasimamia mashindano hayo. 926114