Kituo hicho ni cha pili cha kuchapisha na kusambaza Qur'ani Tukufu nchini Pakistan. Tovuti ya Pakistan Observer imeripoti kuwa kituo hicho ambacho kina mashine za kisasa kabisa za kuchapisha Qur'ani Tukufu, kimefunguliwa katika sherehe iliyohudhuriwa na maulamaa na wahakiki.
Mkuu wa kituo hicho Abdul Malik Mujahid amesema katika sherehe hiyo kwamba inasikitisha kuwa licha ya idadi ya Waislamu kufikia karibu watu bilioni mbili lakini Waislamu hawajafanya jitihada zaidi katika uwanja wa uchapishaji wa Qur'ani Tukufu.
Kituo hicho cha kuchapisha Qur'ani kimefunguliwa kwa lengo la kukabiliana na njama zinazofanywa na wasiokuwa Waislamu kwa ajili ya kuchafua au kupotosha sura safi ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na pia kwa ajili ya kuhudumia Uislamu na Qur'ani Tukufu. 926229