Maafisa wa Msikiti wa Attauba katika mji wa Evere nchini Ubelgiji wamesema kuwa wameazimia kufanya kikao hicho katika siku za mwanzoni mwa mwaka huu mpya wa Miladia.
Lengo la kikao hicho limetajwa kuwa ni kuarifisha sehemu mbalimbali za kitabu kitakatifu cha Waislamu, Qur'ani kwa raia wasiokuwa Waislamu wa mji wa Evere na wamewaalika wakazi wote wa mji huo kushiriki kwenye kikao hicho.
Maulamaa watakaoshiriki katika kikao hicho wataeleza sababu za kuteremshwa aya za Qur'ani Tukufu, nafasi ya Qur'ani katika maisha ya Waislamu na lengo la kuteremeshwa kwake. 926593