IQNA

Qur'ani kubwa zaidi iliyoandikwa kwa hati za mkono yaonyeshwa Kabul

15:18 - January 01, 2012
Habari ID: 2249255
Qur'ani kubwa zaidi duniani iliyoandikwa kwa hati za mkono ilionyeshwa jana katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Pakistan mjini Kabul.
Gazeti la Khaama Press limeripoti kuwa Qur'ani kubwa zaidi iliyoandikwa kwa hati za mkono ilionyeshwa jana mjini Kabul katika sherehe iliyowashirikisha viongozi wa ngazi za juu wa Chama cha Taifa cha Pakistan (Pakistan National Party) na chama cha Awami Pakhtonkhwa na inatazamiwa kuonyeshwa kwa watu wote siku chache zijazo.
Gazeti la Khaama Press limeripoti kuwa nakala hiyo kubwa zaidi ya Qur'ani iliyoandikwa kwa hati za mkono imetayarishwa kwa maagizo ya Kituo cha Utamaduni cha Hakim Naser Khusraw Balkhi kinachoongozwa na Sabir Husseini, imeandikwa na mwanakaligrafia maarufu wa Kiafghani Sayed Mansoor Naderi.
Uandishi wa nakala hiyo ya Qur'ani yenye urefu wa sentimita 230 na upana wa sentimita 150, umechukua kipindi cha miaka mitano. 926326

captcha