IQNA

Kongamano la kila mwaka la Taasisi za Qur'ani mjini Najaf lafunguliwa

16:09 - January 03, 2012
Habari ID: 2250363
Kongamano la kila mwaka la Taasisi za Qur'ani katika mkoa wa Najaf lilifunguliwa jana Jumatatu katika mji huo mtakatifu.
Kongamano hilo limefunguliwa kwa udhamini wa Kituo cha Kitaifa cha Qur'ani Tukufu nchini Iraq. Mashirika na taasisi kadhaa zinazojishughulisha na masuala ya Qur'ani zimeshiriki katika kongamano hilo ambapo Ibrahim Salim, mkuu wa Kituo cha Mafunzo kinachofungamana na Taasisi ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iraq ni mmoja wa watu waliolihutubia.
Ibrahim Salim ametaja baadhi ya malengo ya kongamano hilo kuwa ni pamoja na kutambuliwa vyema changamoto zinazozikabili taasisi za Qur'ani katika mkoa wa Najaf na kuwasilishwa njia za kupambana na changamoto hizo na vilevile kutafuta njia za kuimarisha shughuli za Qur'ani katika mkoa huo.
Amekumbusha kwamba kongamano hilo pia limejaribu kuchunguza shughuli za Qur'ani nchini Iraq na ukweli wa mambo unaotawala katika uwanja huo, kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za Qur'ani na wasomaji Qur'ani katika mikoa yote ya nchi hiyo, kuimarishwa masomo ya Qur'ani na kuzingatiwa zaidi kitabu hicho cha wahyi katika jamii ya Iraq.
Ibrahim Salim amesema uchunguzi wa kuasisiwa Jumuiya ya Qur'ani mjini Najaf kwa mnasaba wa kuchaguliwa mji huo kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu katika mwaka huu wa 2012 ni jambo jingine muhimu lililojadiliwa katika kongamano hilo. 927703
captcha