IQNA

Maonyesho ya sanaa na Qur'ani yafunguliwa Mauritania

15:51 - January 03, 2012
Habari ID: 2250365
Maonyesho ya tatu ya Sanaa na Qur'ani chini ya anwani ya 'Amana Takatifu' yalifunguliwa jana Jumatatu katika jumba la maonyesho ya mambo ya kale huko Nouakchott mji mkuu wa Mauritania.
Maonyesho hayo ambayo yamefunguliwa kwa ushirikiano wa Kituo cha Utamaduni cha Hiraa cha Uturuki, yanatazamiwa kuendelea hadi tarehe 15 Januari.
Picha kubwa za kurasa za Qur'ani Tukufu ambazo zinarejea nyuma hadi katika zama za Mtume Mtukufu (saw) zinaonyeshwa kwenye maonyesho hayo. Picha nyingine muhimu zinazoonyeshwa kwenye maonyesho hayo ni zile zinazohusiana na kilemba cha Nabii Yusuf na fimbo ya Nabii Musa (as).
Mambo mengine yanayoonyeshwa katika maonyesho hayo ni kazi za mikono na kaligrafia ya Kiislamu za Waturuki pamoja na mazingira ya kuvutia ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Kituo cha Utamaduni cha Hiraa kimeandaa vikao mbalimbali vya mijadala na kielimu katika maonyesho hayo kwa shabaha ya kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni kati ya nchi mbili hizo za Kiislamu.
Kituo hicho pia kinaendesha masomo ya masuala ya maktaba katika maonyesho hayo kwa lengo la kuhuisha utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu kwa watafiti na wanachuo walio na hamu ya kunufaika na masomo hayo. 928015
captcha