IQNA

Baraza Kuu la Qur'ani kuanzishwa Iraq

15:41 - January 04, 2012
Habari ID: 2251062
Iyyad al-Kaabi, ustadh wa Kituo cha Kitaifa cha Masomo ya Qur'ani nchini Iraq amesema kuwa Baraza Kuu la Qur'ani litaanzishwa hivi karibuni nchini humo.
Amesema jumuiya za Qur'ani zitaanzishwa katika mikoa yote ya nchi hiyo na kisha Baraza Kuu la Qur'ani kubuniwa. Amesema mipango ya kuzinduliwa jumuiya za Qur'ani katika mikoa miwili ya al-Muthanna na Meisan imekamilika na kwamba jumuiya nyingine kama hizo zimepangwa kuanzishwa hivi karibuni katika mji mtakatifu wa Najaf.
Qassim al-Hulu, mkuu wa Jumuiya ya Qur'ani Tukufu mjini Najaf ameashiria kuanza kongamano la kila mwaka la Taasisi za Qur'ani mjini Najaf hapo siku ya Jumatatu na kuongeza kuwa jumbe mbalimbali za vituo vya kitaifa vya masomo ya Qur'ani vinavyofungamana na Idara ya Wakfu ya Mashia wa Iraq zinashiriki katika kongamano hilo.
Amesema lengo kuu la kufanyika kongamano hilo ni kuanzisha jumuiya za Qur'ani ambazo zitachangia pakubwa katika kuimarisha shughuli za Qur'ani nchini. 928374
captcha