IQNA

Washindi wa mashindano ya hifdhi ya Qur'ani waenziwa Qatar

20:10 - January 04, 2012
Habari ID: 2251500
Washindi wa mashindano ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu ya Annabaa Libaraim al Hudaa makhsusi kwa ajili ya watoto, wameenziwa leo katika taasisi ya Tajul Wiqar nchini Qatar.
Gazeti la al Sharq la Qatar limeripoti kuwa, mashindano hayo yalisimamiwa na taasisi ya Qur'ani ya Tajul Wiqar ya Wizara ya Masuala ya Kheri ya Qatar kwa ajili ya watoto wadogo.
Taasisi ya hifdhi ya Qurani ya Tajul Wiqar ilitayarisha mashindano hayo kwa ajili ya watoto wadogo wenye umri wa kati ya miaka 8 hadi 12 na sherehe za kuwaenzi zimefanyika leo. 928887
captcha