Kwa mujibu wa gazeti la ar-Raya linalochapishwa nchini Qatar taasisi hiyo itatekeleza mpango huo chini ya kaulimbiu ya ' Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Njia ya Uhubiri na Mwongozo Kuelekea Uislamu'.
Akifafanua suala hilo, Ali Abdallah as-Soudi, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Masuala ya Kheri ya Id amesema mpango huo utatekelezwa kwa ushirikiano wa watu wanaojitolea, mashirika na jumuiya za Qatar. Ameongeza kuwa taasisi yake itasaidia kukusanya riali milioni tano za Qatar kutoka kwa wananchi wa Qatar ili kuchangia utekelezaji wa mpango huo.
Amesema tarjumi hizo za Qur'ani kimsingi zitasambazwa katika nchi tofauti ili kuwasaidia watu wasio Waislamu kufahamu mafundisho ya Kiislamu na hatimaye waingie kwenye dini hii tukufu ya mbinguni.
Waandaaji wa mpango huo wanasema kuwa CD za miujiza ya kielimu ya Qur'ani na muhtasari wa maisha ya shakhsia na watu mashuhuri waliosilimu baada ya kusoma aya za Qur'ani Tukufu zitatayarishwa na kusambazwa kama sehemu ya mpango huo kwa wasio Waislamu katika nchi tofauti.
Wanasema kwamba kimsingi tarjumi hizo zitasambazwa katika nchi za Marekani na Ulaya na vilevile nchi nyinginezo zinazozungumza Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kifilipino na lugha ya nyinginezo. 929868