IQNA

Miujiza ya Qur'ani itumike katika afya ya kisaikolojia

15:00 - January 08, 2012
Habari ID: 2253108
Miujiza ya kisayansi na kijamii ya Qur'ani Tukufu inapaswa kutumiwa katika masuala mablimbali ya kielimu, kitiba na kijamii.
Akizungumza na IQNA, Dr. Mohammad Rasuli wa Bodi ya Sayansi ya Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Hormozgan kusini mwa Iran amesema Qur'ani Tukufu ndio chanzo bora zaidi cha ukombozi wa mwanadamu katika nyanja zote za kimwili, kisaikolojia na kiroho.
Akiashiria sayansi ya afya ya kisaikolojia ambayo humsaidia mtu kuwa na uhusiano na dunia inayomzunguka, amesema: "Qur'ani Tukufu ndio marejeo bora na kamili zaidi ya kitengo hiki cha sayansi.".
Dk. Rasuli amesema kuna haja ya vyuo vikuu nchini kuimarisha taaluma ya tiba ya Qur'ani na kuongeza kuwa warsha mbalimbali zinaweza kusaidia katika suala hili. 926574
captcha