Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, gazeti la Al Anbaa la Kuwait limemnukulu Abdullah Barak Mkuu wa kamati hiyo akisema kuwa mashindano hayo yatajumuisha hifdhi, qiraa, na tawjeed ya Qur'ani Tukufu. Amesema mashindano hayo yataanza tarehe 12-30 Aprili mwaka huu ambapo nchi 50 zitashiriki katika ukumbi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Misaada ya Kiislamu Kuwait.
Amesema kikao cha utangulizi kuhusu mashindano hayo kimefanyika ambapo washiriki wametoa mapendekezo ya kuinua kiwango cha mashindano hayo.
Abdullah Barak amesema ripoti kamili kuhusu namna mashindao hayo yatakavyofanyika itatangazwa katika siku zijazo.
Majaji wa mashindano hayo watajumuisha maqarii maarufu kutoka nchi mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu.
930939