Muhammad Mudh'hir ambaye ni miongoni mwa maafisa wa jumuiya ta ICNA amesema kuwa kuna fikra potofu na sura isiyokuwa sahihi kuhusu Qur'ani Tukufu katika jamii ya Marekani na kwamba Waislamu wameanzisha ratiba iliyopewa jina la "Kwanini?" kwa lengo la kufuta sura hiyo chafu inayotolewa kuhusu Uislamu.
Mudh'hir ambaye alikuwa akigawa nakala za Qur'ani na vitabu vya Kiislamu mbele ya Makataba ya Umma wa Santa Margarita huko California, amesema lengo la mpango huo ni kuarifisha sura halisi ya Uislamu na Qur'ani kwa sababu aghlabu ya watu wanafananisha utamaduni wa nchi fulani au kundi makhsusi na dini tukufu ya Uislamu. Ameongeza kuwa watu hao wamekuwa wakisikia habari zisizokuwa za kweli katika vyombo vya mawasiliano na kuzinasibisha kwa Uislamu.
Japokuwa hakuna takwimu rasmi kuhusu idadi halisi ya Waislamu nchini Marekani lakini inakadiriwa kuwa ni kati ya watu milioni 6 na 8. 930884