Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA tawi la Kati mwa Asia, olimpiadi hiyo imeandaliwa na Idara ya Mwakilishi wa Chuo Kukuu cha Kimataifa cha Al Mustafa katika ukumbi wa Chuo cha Kidini cha Khatamul Anbiya. Olimpiadi hiyo ilikuwa na sehemu 12 katika vitengo viwili vya mitihani ya maandishi na simulizi ambapo kulikuwa na washiriki 1700 kutoka maeneo mbalimbali ya Afghanistan.
Akihutubu katika sherehe za ufunguzi wa Olimpiadi hiyo Januari nne Hujjatul Islam Saleh, Mkuu wa Masuala ya Kiutamaduni na Kielimu katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa amesema Waislamu nchini Afghanistan wamekaribisha vizuri mipango ya kiutamaduni ya Iran.
Amesema olimpiadi ya Qur'ani inalenga kuinua utamaduni wa Qur’ani nchini Afghanistan. Ametoa wito wa Waislamu kufuata mafundisho ya Qur’ani Tukufu sambamba na kuhifadhi na kusoma kitabu hicho kitukufu.
Akizungumza katika hafla hiyo, mwanazuoni wa ngazi za juu wa Afghanistan Ayatullah Sayyid Muhsen Hojjat Kabuli amesema kuandaa hafla za Qur’ani huinua fikra za kidini katika jamii.
Washindi katika Olimpiadi ya Qur’ani Tukufu ya Afghanistan watashiriki katika Olimpiadi ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu itakayofanyika nchini Iran.
929808