Gazeti la The Star limeripoti kuwa Mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho la jimbo la Tringano Muhammad Yusuf Abdullah amesema kuwa nakala hiyo ya Qur'ani iliyopambwa kwa dhahabu ni miongoni mwa athari za Kiislamu zinazoonyeshwa kwenye maonyesho hayo yatakayoendelea kwa kipindi cha miezi sita.
Ameongeza kuwa nakala hiyo ya Qur'ani ilitayarishwa miaka 500 iliyopita katika zama za utawala wa kifalme wa Ming.
Muhammad Yusuf amesema kuwa uandishi wa nakala hiyo ya Qur'ani ulianza katika kipindi cha utawala wa Kiothmani kwa kutumia hati za Naskh na baadaye nakala hiyo ilipelekwa mashariki mwa Turkmenistan na mwanazuoni mmoja wa Kiislamu. Ilirejeshwa tena China na kuwekwa katika mkoa wa Yunnan.
Wataalamu wa kimataifa wanasema kuwa nakala hiyo ya Qur'ani ina thamani ya karibu dola milioni 54. 931601