Mtoto mwenye umri wa miaka sita, Umar Abdul Razaq, ameshinda mashindano ya kuhifadhi Qur'ani yaliyoandaliwa hivi karibuni na Jumuiya ya Mujahidun huko Lagos, Nigeria.
Kwa mujibu wa gazeti la Nation la Nigeria, mashidano hayo yalikuwa na washiriki wakubwa zaidi kuliko mshindi.
Abdul Razaq aliyeshiriki katika kitengo cha watoto ni mwanafunzi wa Shule ya Kiarabu na Kiislamu ya Madrassatul Ihyaaul Athar al Mutakkin katika jimbo la Ogun.
Aliibuka mshindi baada ya kusoma sehemu alizochaguliwa za Qur'ani Tukufu.
Kwa mujibu wa mkuu wa Jumuiya ya Mujahidun, Al Haj Abdul Razaq Idris mashindano hayo ambayo ni ya tatu ya aina yake yanalenga kuhimiza usomaji Qur'ani miongoni mwa vijana wenye umri wa chini.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi Umar Abdul Razaq amesema kamwe hatoacha kuisoma Qur'ani na kushiriki katika mashindano hayo.
931798