IQNA

Qur'ani zilizo na makosa ya chapa zakusanywa Imarati

17:02 - February 01, 2012
Habari ID: 2266775
Baraza la Kitaifa la Vyombo vya Habari la Imarati limekusanya nakala za Qur'ani zilizo na makosa ya chapa kutoka soko la mji wa al-Ain.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Imarati WAM, nuskha hizo zimekusanywa katika soko hilo kutokana na kuwa na makosa mengi na vilevile kutofautiana sura zake na utaratibu unaokubalika.
Wataalamu waliopewa jukumu la kufuatilia suala hilo wametambua kwamba nakala hizo zina makosa mengi kama vile ya kukaririwa kurasa kwa kadiri kwamba wasomaji wamekuwa wakichanganyikiwa wakati wa kuzisoma. Wataalamu hao pia wamepata humo makosa kama vile ya kutofautiana maneno na aya zake kinyume na utaratibu unaokubalika.
Baadhi ya maafisa wa baraza lililotajwa wanasema kwamba nakala hizo zilizokusanywa hazikuchapishwa nchini Imarati na kwamba ziliingizwa nchini humo bila kibali kutoka kwa idara rasmi za nchi hiyo.
Akibainisha suala hilo, Muhammad Matar al-Kaabi, Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kiislamu na Wakfu ya Imarati amesema kuwa idara hiyo kila mwaka hushirikiana na makundi tofauti kwa lengo la kuzuia kuingizwa nchini humo nakala zenye makosa ya chapa na kwamba hadi sasa idara hiyo imefanikiwa kuzuia kutawanywa kwa nakala kama hizo katika vituo 70 vya uchapishaji na usambazaji vitabu. 944269
captcha